Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Wydad: Tutafuzu Nusu Fainali, hilo mlitambue

Juan Carlos Garrido Juan Carlos Garrido Fernández

Mon, 24 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Simba katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha mkuu wa Wydad Casablanca, Juan Fernandez amesema kipigo hicho bado hakitoshi kuwahakikishia Wydad kutotinga hatua ya inayofuata ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza mara baada ya mchezo Kocha huyo amesema;

“Tunakwenda nyumbani tuna imani tutafuzu hatua inayofuata. Hali ya hewa ya kucheza saa 10 jioni sio rafiki sana kwetu japokuwa imechangia kwa kiasi chake lakini isiwe sababu, tunajiandaa kwa ajili ya mchezo ujao.”

Simba watakuwa na kibarua kigumu cha kulinda ushindi wao mbele ya Bingwa huyo mtetezi wa Ligi ya Mabingwa Ijumaa hii nchini Morocco.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live