Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Vipers, Presha inapanda presha inashuka

Vipers 7861395 Kocha wa Vipers, Roberto Luiz Bianchi

Sat, 25 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba tayari ipo Uganda kwa ajili ya mechi ya leo Kundi C ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers, huku kocha wa wenyeji, Roberto Luiz Bianchi akiingiwa ubaridi mapema kabla ya mechi hiyo itakayopigwa Jumamosi ya leo mjini Entebbe.

Mechi hiyo ya tatu kwa kila timu kwenye kundi hilo, itapigwa leo kuanzia saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa St Mary uliopo Entebbe na kocha Bianchi alisema itakuwa vita kubwa baina yao, kwani yeye ni kocha mgeni kikosi, wakati mpinzani wake,Roberto Oliveira ‘Robertinho’ akiwa anaijua Vipers.

Akizungumza Bianchi alisema anatarajia mchezo mgumu kutoka kwa wapinzani wao ingawa malengo yao makubwa ni kubaki na pointi tatu kutokana na kutoanza vizuri katika mechi mbili za awali akifungwa 5-0 na Raja Casablanca na suluhu na Horoya AC.

Kocha huyo aliyechukua nafasi ya Robertinho alisema; “Huenda Simba ina faida kubwa wakati huu tunapokutana nayo kuliko sisi kwa sababu kocha wao anaijua vyema timu hii tofauti na mimi ninavyowajua kwani bado sina muda mrefu hapa,” alisema.

Aidha Bianchi aliongeza Simba haifahamu vizuri na ameanza kuiangalia katika michezo yake miwili tu iliyopita ya hatua hii ya Ligi ya Mabingwa huku akisubiri ripoti kamili ya mtathimini wao.

“Matarajio yao yanaweza yakawa makubwa kutokana na uhalisia ulivyo ingawa watakutana na kocha mpya (mimi), mbinu tofauti na aina ya uchezaji na mwisho wa siku tukajikuta wote hali zetu ziko sawa.”

Timu zote zinahitaji ushindi ili kujiwekea mazingira mazuri kwenye kundi lao kutokana na kuanza vibaya ingawa kwa upande wa Simba wao wana kazi kubwa ya kufanya baada ya kupoteza michezo yote miwili.

Simba iko mkiani mwa msimamo wa kundi hilo ikiwa haina pointi yoyote, huku Vipers ikiwa nafasi ya tatu na pointi moja.

Raja Casablanca ya Morocco ndio vinara kwani baada ya kushinda michezo yote miwili iliyopita ya awali imefikisha pointi sita nyuma ya Horoya ya Guinea inayoshika nafasi ya pili na pointi nne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live