Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Ureno aelezea bifu lake na Ronaldo

Fernando Santos X Ronaldo Kocha Ureno aelezea bifu lake na Ronaldo

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa Ureno, Fernando Santos ameelezea ugomvi wake na nyota mkubwa wa taifa hilo, Cristiano Ronaldo ambaye bado anamchukulia kama mtoto wake.

Fernando Santos analaumu kutoelewana na mwanasoka huyo bora Ureno na hawakuwahi kuzungumza tangu alipomwekwa benchi, Ureno ikitolewa na Morocco kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia Qatar miezi 11 iliyopita.

Santos aliliambia Gazeti la A Bola:

“Hatujazungumza tangu nilipokuja Ureno kutoka Qatar. Siku ya mechi, asubuhi nilipoenda kueleza kuwa hatacheza na kwanini hachezi alinielewa vibaya. Uhusiano wetu bado upo pale pale na ataendelea kuwa kama mtoto wangu. Siku akiamua kunipigia simu nitakuwepo kila wakati.” Santos alisema na kusisitiza anamthamini Ronaldo lakini sio kama mchezaji bora duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live