Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Uganda amtaja Novatus Dismas

Novatus Dismas Legalize Kocha Uganda amtaja Novatus Dismas

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Uganda The Cranes, Moses Basena amesifu kiwango kizuri kilichoonyeshwa na mastaa wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars akisema licha ya kupoteza mbele yao, lakini kuna vipaji vipya ambavyo kama vitashikiliwa vitaipaisha nchi kimataifa miaka michache ijayo.

Stars ilipoteza kwa bao 1-0 mbele ya Uganda kwenye mechi ya Kundi F ya kuwania Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) zitakazofanyika mwakani nchini Ivory Coast iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, siku chache tangu iliposhinda ugenini zilipokutana Ismailia, Misri.

Akizungumza mara baada ya pambano hilo, kocha huyo aliyewahi kuinoa Simba alisema soka la Tanzania linazidi kupiga hatua kila siku kutokana na wachezaji wengi kupata nafasi ya kucheza nje ya mipaka ya nchi yao.

"Wachezaji kama Simon Msuva, Novatus Dismas na wengine wengi wameonyesha wana kitu kikubwa sana kwa nchi huko mbeleni kwani ukiwaangalia unaona ni kizazi bora kinachokuja," alisema Basena na kuongeza soka la sasa linategemea vijana na ili upige hatua ni lazima uwaandae huko mbeleni.

"Kwenye timu ni lazima uwe na wazoefu na hata kwetu unaona tunamtumia bado, Emmanuel Okwi lengo ni kutengeneza muunganiko na vijana ili wazidi kujifuza zaidi kutoka kwao," alisema.

Basena anamsaidia Milutin Sredojevic 'Micho' baada ya Charles Livingstone Mbabazi kuitema timu hiyo kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi, huku akiwana kumbukumbu ya kunoa Simba mwaka 2011 japo kwa muda mfupi kabla ya kurudia kwao Uganda alipo hadi sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live