Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Uganda: Kuifunga Tanzania ni tabia yetu

Micho Micho Kocha wa Uganda Cranes, Milutin Sredojevic ‘Micho’

Mon, 5 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Uganda Cranes, Milutin Sredojevic ‘Micho’ amesema kwamba kuifunga Tanzania sasa imekuwa ndiyo tabia ya Uganda.

Micho ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Taifa Stars kwenye mchezo wa mkondo wa pilj wa kufuzu fainali za CHAN za 2023 na kupata ushindi wa jumla wa 4-0.

"Mwaka 2013 tulipowafunga kwa matokeo ya jumla ya 4-1, wapo waliosema tulibahatisha.

Mwaka 2015 tukawafunga tena kwa matokeo ya jumla ya 4-1, wakasema tena tumewabahatisha.

Lakini ushindi huu wa sasa wa matokeo ya jumla ya 4-0 utamaliza yale maneno ya kwamba huwa tunawabahatisha.

Sasa imekuwa tabia yetu."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live