Wed, 13 Sep 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps anasisitiza kuwa Kiungo Paul Pogba hawezi kujihusisha na utumiaji wa Madawa ya kulevya huku akitolea mfano kuwa kipindi cha Chanjo ya Corona Paul Pogba alikataa kutumia akidai kuwa hawezi kutumia Dawa za Chanjo hiyo.
"Hainiingii Akilini mtu kama Pogba kutumia dawa za Kusisimua misuli ni jambo gumu kuliamini kwa sababu Pogba namjua hapendelei madawa kabisa ni kama watu wamepanga kumfanyia Fitina tu"
Pogba anakabiliwa na mashtaka ya kutumia madawa ya kusisimua misuli ambayo yamepigwa marufuku michezoni
Chanzo: www.tanzaniaweb.live