Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Tanzania Prisons azitaka alama tisa Ligi Kuu

Image 146.png Kocha Tanzania Prisons azitaka alama tisa Ligi Kuu

Fri, 5 May 2023 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Maafande wa Magereza ‘Tanzania Prisons’, Abdalah Mohamed ‘Bares’ amesema kikosi chake kitalazimika kupambana kufa na kupona katika michezo mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyosalia.

Tanzania Prisons itacheza dhidi ya Kagera Sugar Mei 7, kwenye Uwanja wa Kaitaba ambapo Kagera Sugar ilitoka kupata ushindi dhidi ya Mbeya City Kwa bao 1-0.

Hadi sasa Tanzania Prisons ina alama 31 baada ya kucheza michezo 27 imetoka kushinda dhidi ya Geita Gold Uwanja wa Nyankumbu.

Kocha Bares aliyekabidhiwa mikoba ya Kocha kutoka nchini Kenya Patrick Omuka Odhiambo mapema mwaka huu, amesema wanahitaji kushinda zaidi michezo hii ya mwisho na kuhakikisha wanabaki Ligi Kuu Bara.

“Ushindani katika ligi ni mkubwa na tunahitaji kushinda katika mechi zetu zilizobaki ikiwa ni pamoja na dhidi ya Kagera Sugar tunawaheshimu wapinzani wetu hivyo tunafanya maandalizi mazuri.”

“Makosa katika mechi zilizopita tunafanyia kazi kikubwa ni Kuona tunakuwa kwenye mwendelezo mzuri wakushinda tutakuwa imara na mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema Bares

Chanzo: Dar24