Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Taifa Stars awaka 'mchezaji akizingua nambadilisha'

Adel Amrouche Kocha Stars Kocha Taifa Stars awaka 'mchezaji akizingua nambadilisha'

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche amesema anahitaji mechi zaidi za kirafiki kukipima kikosi chake lakini pia, haangalii sura ya mchezaji anapopanga kikosi chake.

Kocha huyo ameyasema hayo jana mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Sudan na matokeo kuwa sare 1-1.

"Tunahitaji mchezaji wa kuwa tayari kumalizia kule mbele, tunalinda vizuri, tunacheza vizuri katikati lakini nani anakwenda kumalizia kufunga? Tunahitaji wafungaji, mimi siangalii majina mchezaji wa mbele asipofunga nambadilisha," alisema kocha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live