Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Tabora United atema cheche

Tabora United Www Kocha Tabora United atema cheche

Sat, 23 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha mpya wa Tabora United, Denis Goavec amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya kutua klabuni hapo juzi na kutema cheche akisema yeye ni mtu wa matokeo mazuri na hataki kutibuliwa kibarua chake, huku akiwataka wachezaji na mashabiki kutimiza wajibu wao kwa manufaa ya timu.

Kocha huyo raia wa Ufaransa (66) ataiongoza timu hiyo hadi mwisho wa msimu akichukua mikoba ya Mserbia, Goran Kopunovic aliyetimuliwa katikati ya wiki kutokana na matokeo mabovu ya Ligi Kuu.

Goavec alianza kibarua juzi kwa kusimamia mazoezi ya timu hiyo kujiandaa na mechi za Kombe la Shirikisho la Azam na Ligi Kuu, kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora, akisisitiza utimamu wa wachezaji.

Alisema peke yake hawezi kuipa matokeo mazuri timu hiyo na kurejesha furaha kwa mashabiki bali wachezaji wanapaswa kupambana kutimiza wajibu wao, viongozi na mashabiki kuungana kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha malengo yanafikiwa.

"Watu wasiwe na hofu kwa sababu mimi ni mtu wa matokeo, mtu wa kazi nataka kupata raha nipate tabasamu ndani ya timu, hivyo nitajituma iwezekanavyo kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri". alisema Goavec.

Kocha huyo wa zamani wa AS Vita ya DR Congo na JS Saoura ya Algeria, alisema ni furaha kwake kufanya kazi na timu hiyo na katika siku yake ya kwanza ameridhishwa na utendaji kazi wa wachezaji jambo ambalo ni ishara nzuri kwake.

"Kama mwalimu mpya leo nililenga kuhitaji kufahamu hisia na akili za wachezaji katika kucheza mpira na kuangalia utimamu wao, hivyo mimi na wachezaji tutafanya kazi kwa uhakika kupata kile ambacho mashabiki wanakitarajia" alisema Mfaransa huyo aliyeipokea timu ikiwa nafasi ya 13 ikikusanya pointi 21 kupitia mechi 21, ikishinda mara nne tu na kupioteza15 na kuambulia droo tisa.

Chanzo: Mwanaspoti