Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha TP Mazembe: Usiombe kukutana na Mamelodi Robo Fainali

Kocha Mazembeeee Kocha Mkuu wa TP Mazembe, Lamine N'diaye

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa TP Mazembe, Lamine N'diaye amesema kuwa ubora wa Mamelodi Sundowns ni mkubwa sana hivyo siyo timu ya kuomba kukutana nayo kabisa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwani hata yeye anaiogopa

"Kwa upande wetu hakuna Timu nyengine yoyote ile inayoweza kutusumbua au kutupa presha kama tuliyopata kutoka kwa Mamelodi huku katika hatua ya Makundi, furaha yetu ni kutokukutana nao katika hatua ya Robo Fainali.."

"Yoyote yule tutakayepewa Robo Fainali tunaweza kummudu na kumfunga pia ilimradi hatokuwa Mamelodi Sundowns.."

"Nimeanza kuzeeka nafikiri na hii inamaanisha mimi ni mmoja wa watu waliobahatika kushuhudia Timu bora nyingi Afrika katika kila nyakati na ninadiriki kusema hii Mamelodi ya sasa sio yakuombea kukutana nayo popote pale.. hata Timu za magharibi zitaniunga mkono kwa maneno haya.. omba vyote ila usiombe kupewa Mamelodi kwenye mechi za maamuzi kwasasa."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live