Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha TMA achekelea Championship

Kocha TMA Kocha TMA achekelea Championship

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya timu zote zinazoshiriki Ligi ya Champioship kucheza mechi Tano kila mmoja hadi sasa kocha wa TMA Stars,Ngawina Ngawina amefunguka kuridhishwa na mwendendo wa timu yake.

Maafande hao kutoka Chuo cha Maofisa wa Kijeshi Tanzania katika msimamo wako nafasi ya pili kwa alama 11,baada ya kushinda mechi tatu na kutoka sare michezo miwili huku ikifunga goli nne na kuruhusu nyavu zao kuguswa mara moja.

Timu hiyo ilianza kwa sare tasa dhidi ya Stand United,kisha ikashinda 1-0,kwa Biashara United,ikatoka tena sare tasa na Cosmopolitan alafu ikaichapa 2-1 Pan African na kuing’uta maafande wenzao Mbuni FC 1-0.

Ngawina akipiga story na Mwanaspoti alisema kuwa katika mechi hizo tano aliweka mikakati ya kuchukua alama zote 15 lakini amepata 11 amekosa nne siyo mbaya,huku akiwapongeza vijana wake kwa kupambana.

Alisema kwa namna kikosi chake inavyocheza kama mwalimu kwa kweli kinamridhisha hasa baada ya kufanyia kazi kwenye uwanja wa mzoezi mapungufu kadhaa ambayo yalikuwepo na anaamini kama wataendelea kucheza hivi kwa kujituma katika kila mechi timu itapanda Ligi Kuu.

“Ligi ni ngumu na kila siku tunacheza na timu tofauti sisi ni timu ngeni lakini malengo ni moja kwenda Ligi sasa tutaendaje lazima vijana wajitume hivi ili kufanikisha ilo”,alisema Ngawina.

Aliongeza kuwa nguvu zote sasa anaezielekeza katika mechi mechi mbili mfululizo nyumbani dhidi ya Mbeya Kwanza ambayo itapigwa Oktoba 14 na Ruvu Shooting ambayo itachezwa Oktoba 23 ambazo kwao ni muhimu kushinda ili kuendelea kusalia juu kwenye msimamo.

Alitumia fursa hiyo pia kuipongeza uongozi kwa namna ambavyo imekuwa bega kwa bega na wachezaji kwa kuwatia morali ambayo imekuwa ni faida kubwa kwao hasa katika kuendelea kuipambania malengo ya timu.

“Hatupaswi kubetweka na matokeo haya Ligi ni ndefu kila timu inataka kupanda Ligi Kuu,tutaendelea kucheza hivi hivi na niwaombe mashabiki wa Soka Arusha wasituchoke waendelee kutuunga mkono tutawafuarahisha”,alisema Ngawina.

Chanzo: Mwanaspoti