Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Sven aaga rasmi Wydad

Sven Apewa Mtihani Wydad.png Kocha Sven aaga rasmi Wydad

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Wydad Casablanca, Sven Vandenbroeck rasmi ameachia ngazi baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miezi miwili pekee.

Sven ambaye ni raia wa Ubelgiji na aliwahi kuifundisha Simba Sc ya Tanzania kabla ya kutimka, alijiunga na Wydad mwezi mei mwaka huu akiokea FAR Rabat ya hapo hapo Morocco lakini ameshindwa kuipa Ubingwa wa Afrika na Ubingwa wa Botola League ya Morocco.

Ndani ya wiki kadhaa, Sven alipoteza mataji yote aliyokuwa akiwania ikiwemo Ubingwa wa Morocco ambao ulichukuliwa na timu aliyokuwa akiifundisha awali ya FAR Rabat wakati akishindwa pia kunyakua Ubingwa wa Afrika baada ya kukubali kichapo cha Al Ahly kwenye mchezo wa fainali.

“Ni muda mfupi lakini wa muhimu. Ni shukrani kubwa na kwa heri familia muhimu,” amesema Sven ambaye anahusishwa kujiunga na CR Belouizdad ya Algeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live