Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Stars awatema Fei Toto, Kapombe na Tshabalala

Kapombe , Fei, Zimbwe Kocha Stars awatema Fei Toto, Kapombe na Tshabalala

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Taifa Stars Adel Amrouche ameendelea kuwapotezea kiungo wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto' na mabeki wa Simba wa pembeni Mohamed Hussein 'Tshabalala' na Shomari Kapombe.

Katika orodha ya wachezaji 28 wa Stars inayokwenda kucheza dhidi ya Sudan kwenye mchezo wa kirafiki wa Kalenda ya Shirikisho la Soka Dunaini (FIFA) Amrouche pia amemtema kiungo wa Yanga Jonas Mkude.

Orodha hiyo imewajumuisha makipa Beno Kakolanya (Singida Big Stars), Metacha Mnata (Yanga), Ally Salim (Simba).

Mabeki ni Israel Mwenda(Simba),Abdulrazak Hamza(Super Sport United), Nickson Kibabage, Ibrahim Hamad, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job (wote Yanga), Abdi Banda( Richards Bay),Haji Mnoga (Aldershot Town)

Viungo waliojumuishwa ni Kibu Denis, Mzamiru Yassin (wote Simba),Mudathir Yahya (Yanga), Abdul Seleman (Azam), Baraka Majogoro (Chippa United), Abdulmalik Zakaria (Namungo), , Sospeter Bajana(Azam), Himid Mao (Tala'ea El Gaish), Ben Starkie (Basford United), Morrice Abraham (FK Sportak Subotica).

Washambuliaji ni Mbwana Samatta( Paok FC), Simon Msuva ( JS Kabylie), Clement Mzize (Yanga), Said Khamis (FK Jedinstvo), George Mpole (FC Lupopo) na Nassoro Saadun (Ihefu).

Starsa itaondoka nchini kesho ikielekea Saudi Arabia itakapocheza dhidi ya Sudan, mchezo utakaofanyika Oktoba 15.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live