Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Stars alia wachezaji kukosa namba kwenye Klabu zao

Wachezaji Stars Wachezaji wa Taifa Stars

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania leo kimesafiri kuelekea nchini Morocco kwaajili ya mchezo wa kwanza wa kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia 2026 dhidi ya Niger.

Wakati wa maandalizi kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa amesema hakutakuwa na uwezekano wa kuwa na timu ya Taifa nzuri kama wachezaji wanaotegemewa wanakaa benchi kwenye klabu zao.

"Kinachosikitisha tuna wachezaji wengi ambao hawachezi kwenye klabu zao. Klabu hazitusaidii, tunaweza vipi kuwa na timu nzuri ya Taifa kama wachezaji wazuri kwenye timu ya Taifa wanakaa benchi".

Upi mtamo wako, anachokisema mwalimu kina uhalisia au ana jitetea kabla ya mambo kuharibika ?.....

Chanzo: www.tanzaniaweb.live