Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Stars afanyie kazi mambo haya mawili dhidi ya Algeria

Adel Amrouche Stars Kocha wa Taifa Stars, Adel Amrouche

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" Saa 4:00 usiku watakuwa na kibarua dhidi ya vinara wa kundi Algeria wakipigania nafasi ya kufuzu mashindano ya AFCON mwakani.

Stars wanahitaji angalau alama moja katika mchezo huo ili kujikatia tiketi ya kwenda Ivory Coast mwakani.

Algeria sio watu wa kawaida hata kidogo hivyo ili kupata ushindi ama sare kunahitajika kazi ya ziada na kuna mambo mawili Stars wanapaswa kuyatilia umakini wa hali ya juu dhidi ya Algeria.

1.Kucheki begani na kuzungumza sana ikitokea mpinzani kashafanikiwa kuwapunguza watu na kuingia maeneo hatari...Mnaweza kuwa wengi na mkahisi mnawaona maadui walipo lakini mkavutwa alafu atatafutwa mtu ambae kajitega tu nyuma yenu au kakimbia late kukutana na mpira kafunga!

2.Wapunguze papara zikitokea nafasi! Ni mara ngapi nafasi zinakuwa chache kwenye mechi alafu mtu anafanya shambulizi kama anatamani liishe tu.

Mwisho wa siku tuzidiwe kwa mengine kama ni uwezo binafsi lakini sio kwenda na maradhi yanayotibika, Muarabu akaenda kututilia ubani tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live