Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Stand United atupiwa virago

Stand United Kocha.jpeg Kocha Stand United atupiwa virago

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya @standunitedfc 'Chama la Wana' yenye maskani yake Shinyanga, imemfuta kazi kocha wake mkuu Zulkifri Iddy, kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu hiyo inayoshiriki ligi daraja la kwanza (NBC Championship).

Hadi sasa Stand United FC imecheza michezo sita, imeshinda miwili, sare moja na kupoteza mitatu, ikiwa na alama 7 nafasi ya 11 kwenye msimamo.

Stand United FC inakuwa timu ya pili ya NBC Championship msimu huu kumfuta kazi kocha wake, baada ya FGA Talents FC ya mjini Morogoro iliyomfuta kazi Flugence Novatus

Chanzo: www.tanzaniaweb.live