Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Singida agundua tatizo

Hhhhhhhh Kocha Singida agundua tatizo

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kukiongoza kikosi chake kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, kocha mkuu wa Singida Big Stars, Mbrazil, Heron Ricardo Ferreira amesema anapambana kupunguza makosa kwenye eneo lake la ulinzi ili kuhakikisha inawapa nguvu washambuliaji.

Ferreira ameanza na ushindi huo baada ya kukabidhiwa timu hiyo ikiwa imeshinda mchezo mmoja dhidi ya Mtibwa Sugar 1-0 suluhu mbili na kupoteza mechi mbili wakianza na Tanzania Prisons (0-0), Tabora United (0-0), Azam FC (2-1), Mtibwa Sugar (0-1), Simba (2-1).

Akizungumza alisema; “Timu inawachezaji wazuri na wote wanapambana hivyo kazi iliyobaki kwangu ni kuhakikisha naandaa kikosi cha ushindani wa namba kulingana na ubora wa mchezaji mmoja mmoja;

“Nafurahi timu inaonyesha kuwa na uhitaji inapambana kutengeneza nafasi na kufunga shida ipo kwenye ulinzi wanawanyong’onyesha washambuliaji ambao wanafunga na mabao yanarudi kutokana na ulinzi kukosa umakini.” alisema.

Ferreira alisema matokeo mazuri waliyoyapata ni mwanzo mzuri kwake kutambua nini kiongezwe kikosini na kusawazisha makosa yaliyotokea kwenye eneo lake la ulinzi.

Chanzo: Mwanaspoti