Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Singida: Kesho tunawafunga Simba

Kocha Singida Kocha Singida: Kesho tunawafunga Simba

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Msaidizi wa Singida Fountain Gate, Nizar Khalfan amesema mechi ya kesho dhidi ya Simba haitakuwa ya kitoto, lakini ana uhakika wa ushindi kwa maandalizi waliyofanya.

Mbele ya wanahabari leo, Nizar amesema hawaitazami kama mechi ya kisasi bali wanachojua ni kwenda kushinda...

".....hata wao wanajua shughuli yetu, wakikutana na sisi huwa si mechi ya kitoto.....na wangeambiwa wachague kati yetu na Azam kwenye hatua hii nadhani wangechagua kukutana na Azam na siyo Singida"

Je, mechi ikifikia hatua ya penati kama ilivyokuwa kwenye Ngao Jamii 2023 itakuwaje!!? Njzar amesema:-

"Kama tukitoka sare dakika 90 , basi wao watatoka kwa penati...."

Kuhusu 'utajiri' wa washambuliaji walionao, Nizar amesema haiwapi ugumu benchi la ufundi bali inawarahisishia kazi kwakuwa yeyote anayeanza anatimiza wajibu wake, jambo ambalo ni hamasa kwa wanaoanzia benchi.

Je, nini kinawapa jeuri ya kushinda mechi ya kesho...wamepata dawa gani ya kuifunga Simba!!? Nizar amejibu :-

"Hatuwezi kutoa siri"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live