Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Van De Pluijm amesema licha ya Ligi Kuu kubakisha michezo miwili ili kumaliza msimu huu, lakini nyota wake bora hadi sasa ni mshambuliaji na kinara wa mabao wa Yanga na Ligi Kuu, Fiston Mayele.
Kauli ya Pluijm inajiri siku chache tu tangu nyota huyo afunge bao katika ushindi wa 1-0 na kuitoa Singida Big Stars kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), uliopigwa katika Uwanja wa Liti mjini Singida.
“Ukiniuliza mimi nitakwambia anastahili mchezaji bora wa msimu kwani anajua kufunga, ana spidi na anaweza kujiweka katika mazingira mazuri uwanjani, hivyo kwangu binafsi ni mshambuliaji aliyekamilika,” alisema.