Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Simba atia neno kiwango cha wachezaji wake

Pablo Franco Word Kocha wa Simba, Pablo Franco

Sat, 25 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuigaragaza KMC magoli ya kutosha katika mchezo wa Ligi Kuu Bara Disemba 24, Kocha wa Simba Pablo Franco hakusita kuwapongeza wachezaji wake.

Pablo amesema kuwa kwa hali waliyokuwa nayo na kile ambacho wachezaji wamekifanya uwanjani hana shaka ni kazi kubwa iliyofanyika.

"Ushindi wa leo kwangu una thamani kubwa kwa sababu kwa hali tuliyokuwa nayo, kurudi na kucheza kwenye kiwango kama hiki ina maana sana. Kiwango cha Timu kilikua kikubwa kama ukiniambia nitoe alama nitaweka 10 kwa 10".

Katika mchezo huo Simba iliibuka na ushindi wa magoli 4-1 yaliyofungwa na walinzi Mohammed Hussein, Joash Onyango na Kibu Denis aliefunga magoli mawili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live