Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Simba atangaza wiki Sita za moto

Fadlu Davids Misriii Kocha Simba atangaza wiki Sita za moto

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Simba, Fadlu Davids ametamba kuwa baada ya wiki sita za maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya, timu yake itakuwa moto wa kuotea mbali.

Amesema hadi sasa, wameshakamilisha wiki tatu za maandalizi hivyo wamebakiza nyingine tatu za kukamilisha na kutengeneza makali yao.

Kocha huyo anasema kuwa usajili uliofanyika ni wa wachezaji wazuri ambao wamekuwa na uelewa wa haraka wa kile ambacho wanaelekezwa.

“Kwanza kabisa nipongeze mfumo wa usajili, bodi ya klabu na rais kwa usajili. Nadhani tumesajili kikosi kizuri, cha umri mdogo na chenye nishati. Kikosi ambacho kina wachezaji 14 wapya wakiungana na wengine 14 waliokuwepo.

“Ni wachezaji wenye vipaji vizuri na wana kitu cha kuonyesha watakuwa wachezaji wakubwa kwa klabu. Hiyo ndiyo maana ya balansi ya kikosi, kuna sehemu chache ambazo tunaziangalia lakini tuna balansi nzuri kwenye kikosi ambayo inaendana na aina ya soka tunalohitaji kucheza.

Kocha Fadlu alisema kuwa wamebakiza wiki tatu za kumalizia kazi ya kujenga kikosi tishio msimu ujao.

“Mimi ni kocha ambaye siwezi kutofautisha ufiti na mbinu. Hivyo kuanzia siku ya kwanza tulianza kufanyia kazi maandalizi ya kimbinu. Tulianza kwa haraka kufanyia kazi jinsi gani tunacheza.

Baada ya wiki sita tutakuwa tayari kuona wachezaji wakiwa na staili ya kiuchezaji ambayo nataka kuiona. Unaweza kuona mwisho wa mapumziko ya Fifa tutakuwa na mzunguko kamili na kutakuwa na ushirikiano unaoendelea wa jinsi ya kutaka kucheza na hatua kwa hatua kutoka upande wa maandalizi ya kimwili na ya kiufundi,” alisema Fadlu.

Akizungumzia mechi ya kilele cha tamasha la Simba Day dhisi ya APR kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Davids alisema kuwa anautazama kwa malengo mawili ambayo ni kuangalia kiufundi walipofikia katika maandalizi yao na kufurahisha mashabiki.

“Tumeanza wiki ya nne (ya maandalizi). Kuhusiana na utayari na kujiandaa bado tunaendelea lakini tunachukulia mechi kwa pointi ya kwanza ya maandalizi ya msimu mpya lakini pia ni fursa kwa mashabiki kufurahia utambulisho wa wachezaji na benchi la ufundi,” alisema kocha huyo.

Chanzo: Mwanaspoti