Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Simba ataka Chama atimuliwe

Realclatouschama Kocha Simba ataka Chama atimuliwe

Fri, 29 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa Simba SC, Patrick Phiri raia wa Zambia amesema klabu ya Simba inapaswa sasa kufikia hatua ya kuachana kabisa na mchezaji Clatous Chota Chama, ili kulinda heshima na maslahi ya klabu.

Chama pamoja na Nassoro Kapama, walitajwa hivi karibuni kuwa na makosa ya kinidhamu na hivyo kupelekea kusimamishwa kwao klabuni.

Patrick, amesisitiza inapaswa haraka sana jambo hilo la chama liwasilishwe kwenye kamati ya nidhamu ya Simba, ambayo ipo chini ya Kamanda mstaafu wa Jeshi la Polisi, Seleman Kova, ili jambo hilo kushuhulikiwa na kupata muafaka. Kama utakumbuka kamati hii chini ya Kova, iliwahi kushuhulikia masuala tofauti ikiwemo lile la Jonas Mkude, ambae kwasasa yupo Yanga SC.

Phiri, aliongezea kwa kusema licha ya kwamba Chama ni mchezaji mzuri ila nyakati hupita, ubora huisha na kubaki uzoefu tu kiuchezaji na hivyo klabu hiyo inapaswa kufikia maamuzi magumu zaidi, kwakua pia hata suala hilo linaweza kumtoa zaidi mchezoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live