Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Simba atajwa Coastal

Kopunovic Picfdd Kocha Simba atajwa Coastal

Sun, 18 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa Simba, Goran Kopunovic na Javi Martinez raia wa Mexico mmoja wapo huenda akatua kwa Wagosi wa Kaya (Coastal Union) msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Goran raia wa Serbia aliwahi kuifundisha Simba msimu wa 2015/16 wakati Javi yeye aliwahi kuifundisha Vipers ya Uganda pamoja na timu ya Taifa ya Burundi akiwa kama kocha msaidizi.

Imeelezwa kuwa pia katika mchakato huo wa kupata kocha mkuu ambaye atasaidiana na kocha wa sasa Fikiri Elias alikuwepo Abdihamid Moalin aliyewahi kuifundisha Azam FC ila amepigwa chini. 

Chanzo hicho kimeliambia Mwanaspoti kuwa, mchakato huo unaendelea ingawa sasa wamebaki wawili Goran na Javi ambao wanajadiliwa na kama mambo yataenda vizuri basi mmoja wao ataungana na Fikiri msimu ujao.

"Vikao vya ndani vinaendelea, tunaimarisha Benchi la Ufundi kwa ajili ya msimu ujao, tunataka kuwa na kocha mkuu wa kigeni ila Fikiri ataendelea kuwepo kama kocha msaidizi. Hadi sasa kuna majina mawili (Goran na Javi) ambayo tunayajadili," kilisema chanzo hicho

Katika hatua nyingine, uongozi wa klabu hiyo upo kwenye mpango wa kupunguza matumizi msimu ujao ikielezwa mpango huo utaanza kwa kuwaondoa baadhi ya wachezaji wa kigeni.

"Bajeti imekuwa kubwa sana, tumetumia zaidi ya Sh 300 milioni kwa ajili ya gharama zote za wachezaji wa kigeni, kuanzia usajili na vibali vyao vyote (makazi, kazi na TFF), hivyo tumeona tubaki na wachache." kilisema chanzo hicho kutoka ndani ya Coastal Union.

Wachezaji wenye uhakika wa kubaki msimu ujao ni wanne huku watano wakivunjiwa mikataba yao na kwamba mpango wao mkubwa ni kubaki na wazawa zaidi.

Alipotafutwa Msemaji wa timu hiyo, Jonathan Tito kuzungumzia juu ya mipango yao hiyo alisema; "Hii ni klabu ambayo ina utaratibu wake, hivyo kila kitu kitawekwa wazi muda ukifika, kama kuna mabadiliko ya benchi la ufundi, mambo ya bajeti na usajili vyote muda ukifika vitaelezwa kama vitakuwepo."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live