Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Simba ahitimu kozi ya Ukocha ya CAF

Matola Shule Kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola (kushoto)

Sat, 30 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wetu msaidizi Seleman Matola ni miongoni mwa washiriki 25 waliohitimu kozi ya Diploma B ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) iliyofungwa mkoani Morogoro.

Matola amesema anashukuru kwa kumaliza salama kozi na anarejea kikosini kuongeza nguvu katika benchi la ufundi kuelekea michuano iliyo mbele yetu.

Matola ameendelea kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani katika kila mchezo ili kuwapa sapoti wachezaji huku akiwashukuru kwa jinsi walivyokuja katika mechi iliyopita dhidi ya Polisi Tanzania.

“Namshukuru Mungu tumemaliza kozi salama na nimerejea kuungana na benchi la ufundi tayari kwa mapambano yaliyo mbele yetu, kikubwa ninachoomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kwenye mechi zetu kutupa sapoti,” amesema Matola.

Matola ataungana na kikosi katika mazoezi ya mwisho ya kesho ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union Oktoba 31 yatakayofanyika Uwanja wa Boko Veterans na Jumapili atakuwepo kwenye benchi la ufundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live