Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Simba: Waswana Hawafiki dk 45

Simba 10 Kikosi cha wekundu wa Msimbazi

Fri, 22 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Kocha wa Makipa wa Simba, raia wa Brazil, Milton Nienov, amefunguka kuwa, pamoja na kikosi hicho kupewa muda wa mapumziko ya siku mbili, baada ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy FC ya Botswana, wana uhakika mkubwa wa kushinda ndani ya dakika 45 za kwanza.

Simba itashuka kwenye mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Jumapili hii katika dimba la Mkapa, Milton ameweka bayana hayo baada ya kuwepo wa maneno kutoka kwa baadhi ya mashabiki wakiona kitendo cha kikosi hicho kupumzika, kinaweza kuwaondoa kwenye ubora wao, baada ya kushinda mabao 2-0, katika mchezo wa awali uliopigwa Oktoba 17, mwaka huu nchini Botswana.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Milton amesema, tayari kikosi kipo kambini na kinafanya mazoezi yake katika Uwanja wa Boko Veteran nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Amesema ratiba yao ya mazoezi ipo sambamba na mipango ambayo ni sahihi kabisa kuelekea kwenye mchezo huo, ambao wana matumaini ya kuibuka na ushindi mkubwa zaidi ya ule wa Botswana.

“Tayari tumeanza mazoezi baada ya mapumziko ya siku mbili, kikubwa nawaomba mashabiki zetu wawe na imani kubwa na timu yetu kwani mapumziko haya hayaathiri chochote kwenyeushindi wetu na malengo mapya ya ushindi wa mchezo ujao.

“Tuna matumaini kuwa tunaenda kushinda kwa kishindo kwani morali tuliyonayo siyo ya kawaida, hivyo kocha Gomes amefanya jambo zuri kutoa mapumziko maana safari haikuwa ndogo hata presha ya mchezo huo ilikuwa kubwa zaidi ya ushindi tuliopata na Jumapili tuna uhakika wa kuwafunga ndani ya dakika 45 tu za mwanzo,” amesema Milton.

Chanzo: globalpublishers.co.tz