Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Prisons afichua siri

Prisons Lake Tanganyika.jpeg Kocha Prisons afichua siri

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuvuna pointi saba kwenye mechi tatu alizoiongoza Tanzania Prisons, kocha mkuu wa, Hamad Ally amesema kujituma na kufuata maelekezo kwa wachezaji ndio siri ya mafanikio, huku akidai kazi bado.

Prisons haikuwa na mwanzo mzuri kutokana na matokeo yasiyoridhisha hadi kufikia hatua ya kuachana na aliyekuwa kocha wake mkuu, Fredy Felix ‘Minziro’.

Tangu alipojiunga na timu hiyo, Ally ameiongoza michezo mitatu ikiwa ushindi ni mechi mbili dhidi ya Dodoma Jiji na Mashujaa kisha kupata suluhu mbele ya Ihefu na kupanda hadi nafasi ya 10 ikiwa na pointi 14.

Kocha huyo aliliambia Mwanaspoti matokeo hayo si mabaya sana kutokana na walipotoka akieleza bado kazi ni ngumu, lakini upo mwanga za wa kuwafikisha pazuri.

Alisema siri kubwa ya mafanikio kwa muda mfupi ni wachezaji kuelewa falsafa yake, lakini hata kujituma na kupambana kwa kiu ya kutaka ushindi pamoja na sapoti ya mashabiki.

“Siyo mwanzo mbaya, lakini lazima tuendelee kupambana kwa sababu hatujawa pazuri sana inahitaji mwendelezo wa kushinda niwapongeze vijana kwa kazi nzuri na kuelewa nini cha kufanya,” alisema Ally.

Kocha huyo aliongeza kuwa kwa sasa wanarejea nyumbani kwenye Uwanja wa Sokoine kujiandaa na mchezo wa Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) dhidi ya TRA kuhakikisha wanafanya vizuri na kufuzu hatua inayofuata.

“Kila mchezo una umuhimu wake hatuwezi kudharau timu, tunaenda kujiandaa na mchezo huo tukihitaji ushindi na kufuzu hatua inayofuata, tunaomba nguvu na sapoti ya mashabiki,” alisema kocha huyo.

Chanzo: Mwanaspoti