Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Prison awapigia hesabu kali Yanga, "tumejipanga"

Prisons Point 3 Kocha Prison awapigia hesabu kali Yanga, "tumejipanga"

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Yanga ikiwa uwanjani leo kucheza dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa kiporo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex, wapinzani wao Tanzania Prisons wameapa kuondoka na pointi tatu muhimu pindi timu hizo zitakapokutana.

Timu hizo zitakutana Februari 11, kwenye Uwanja wa Sokoine jijini hapa huku Prisons ikiwa haijafungwa katika michezo minne iliyopita ya Ligi Kuu Bara na kati yake imeshinda mitatu na kutoka sare mmoja ikiwa nafasi ya tisa na pointi 17.

Akizungumzia maandalizi yao, kocha mkuu wa timu hiyo, Ahmad Ally alisema wamekuwa na muda wa kutosha wa kujiandaa dhidi ya wapinzani wao, hivyo kwa mbinu zilizotumika katika michezo iliyopita ndio hizo watakazozitumia kwa Yanga pia.

“Sisi tunaendelea na mazoezi tukiwasubiria, tumekuwa na muda mwingi wa kujiandaa na tunaamini tutashinda mchezo huo kwa sababu morali ya wachezaji kufanya vizuri ni kubwa hivyo tunawaheshimu sana ila hatuwaogopi kukabiliana nao,” alisema.

Nahodha wa timu hiyo, Jumanne Elfadhili alisema mchezo huo ni kama michezo mingine na wao wamejiandaa vya kutosha.

“Tumekutana nao mara nyingi na rekodi zinatofautiana ila msimu huu tunahitaji ushindi katika kila mechi, waje wakiamini hii ni Prisons mpya ambayo ina mipango yake,” alisema.

Chanzo: Mwanaspoti