Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Prison ahaha kisa Yanga, ajipanga kuwakabili

Kocha Prisons Ss Kocha Prison ahaha kisa Yanga, ajipanga kuwakabili

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha mkuu wa Tanzania Prisons, Ahmad Ally, amesema wameiangalia vyema Yanga katika mechi mbili ilizocheza na kubaini wapinzani hao ni hatari katika dakika tano za mwisho akitahadharisha nyota wake kuwa makini.

Prisons inawakaribisha Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Sokoine jijini hapa ukiwa wa kufunga mzunguko wa kwanza huku kila timu ikihitaji ushindi kujiweka pazuri.

Yanga inayoongoza ligi hiyo kwa pointi 37, katika mechi tatu ilizocheza mfululizo za viporo, imekusanya pointi saba ikiwa ni ushindi michezo miwili dhidi ya Dodoma Jiji 1-0 na Mashujaa 2-1 na suluhu dhidi ya Kagera Sugar na sasa kituo kinachofuata ni Sokoine.

Katika mechi ilizoshinda Yanga ilipata bao la ushindi katika dakika za mwisho huku mabao yote yakiwekwa wavuni na kiungo mshambuliaji, Mudathir Yahya akianza na Dodoma Jiji dakika ya 87 na Mashujaa dakika ya 85.

Kocha huyo aliliambia Mwanaspoti kuwa wanahitaji kucheza mechi hiyo kwa umakini na tahadhari kuanzia dakika awali hadi mwishoni akisema kuwa wameangalia mechi za wapinzani na kugundua wapi pa kuwashika.

“Mechi ni dakika 90 lazima tuwe makini kwa muda wote, nimeona matokeo yao yanapatikana mwishoni hivyo vijana wanapaswa kupambana na kwa maandalizi tuliyofanya naamini tutashinda.

“Yeyote Yanga anaweza kufanya lolote muda wowote licha ya kwamba Mudathir ndiye amefunga mabao hayo dakika za mwisho ila tutapambana na kila mmoja, nafurahia wachezaji wangu wanavyoonyesha kiwango na ushirikiano,” alisema kocha huyo.

Prisons ipo nafasi ya tisa kwenye msimamo ikiwa na pointi 17, huku Yanga ikiwa ya kwanza na pointi 37.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: