Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Power Dynamos: Simba waongeze kiwango

KOCHA POWER DYNAMOS MWENYA Chipepo Mwenya.

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Power Dynamos, Chipepo Mwenya ametoa ushauri kwa Simba kuwa wafanye kazi ya ziada baada ya kufuzu hatua ya makundi ya kwa sababu wameingia hatua ngumu zaidi.

Chipepo amesema hayo jana mara baada ya kutoka sare na Simba ambao wamefanikiwa kutinga hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kanuni ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya bao 3-3.

“Nachoweza kusema ni kwamba tumejifunza vitu vingi kwenye mashindano haya, tumepoteza nafasi nyingi, hatukuzuia vizuri nab ado tumejifunga wenyewe. Siwezi kuzungumzia marefa, nao ni binadamu wana mafanya makossa kama wanadamu wengine, tumepoteza na hata kama nikizungumzia marefa tayari matokeo yatabaki vilevile.

“Simba wanatakiwa wapambane, sasa hivi wamekwenda group stage ambako ni kugumu zaidi, kifupi wanatakiwa wafanye kazi kubwa kuongeza kiwango chao.

“Tumecheza vizuri vipindi vyote, ila ni baadhi ya wachezaji wetu walipoteza tu umakini tukajifunga wenyewe. Lakini naweza kuwapongeza wamefanya kazi nzuri. Simba wana wachezaji wazuri, wamecheza kama timu ndiyo maana wamepata bao moja,” amesema Mwenya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live