Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Polisi Tanzania njia panda

Kocha Polisi Tanzania Polisi Tanzania yamtimua kocha

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imeisha hiyo. Ndivyo unaweza kusema kwani baada ya taarifa nyingi za kuondoshwa kwa Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Joslin Bipfubusa hatimaye leo katupiwa virago.

Habari za kuaminika kutoka chanzo ndani ya klabu hiyo zimeeleza kuwa mabosi wamemaliza na Mrundi huyo leo kuwaaga wachezaji.

Kwa muda mrefu Bipfubusa amekuwa akitajwa kuondoshwa kutokana na matokeo tasiyoridhisha baada ya kusimamia michezo saba bila ushindi wowote.

Imeelezwa kuwa mapema leo Oktoba 17, mabosi wa timu hiyo wamefikia makubaliano rasmi na Kocha huyo kusitisha kibarua chake na tayari Mrundi huyo amewaaga wachezaji.

Timu hiyo ambayo inaburuza mkia kwa pointi mbili, umeweka kambi yake jijini Mbeya ambapo katika katika mazoezi ya leo ilishuhudiwa Kocha wa viungo, John Tamba akisimamia matizi hayo.

Ikumbukwe Maafande hao wanajiandaa kuwakabili Namungo, mchezo ambao utapigwa uwanja wa Sokoine Mbeya Jumatano ya wiki hii ikiwa ni mechi ya raundi ya nane .

Akizungumzia taarifa hizo, Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Robert Munisi amesema bado Kocha huyo wanaye na suala la kutokuwapo mazoezini leo ni kutokana na matatizo yake binafsi ya kiafya.

"Hata Kocha Msaidizi, Agustino Damian naye anaumwa hata huyo ana matatizo ya kiafya ila kesho atakuwapo kama kuna taarifa nyingine sijaambiwa chochote kwakuwa viongozi wa juu wapo makao makuu Dodoma" amesema Munis.

Kigogo huyo ameongeza kuwa timu hiyo itaendelea kuwapo jijini hapa baada ya mchezo dhidi ya Namungo kujiwinda tena na mechi na Tanzania Prisons, Oktoba 25 utakaopigwa uwanja wa Sokoine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live