Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Pluijm ameeleza kuwa ushindani wao dhidi ya Azam FC kwenye kumaliza nafasi ya tatu iliwafanya wasitishe masuala ya usajili kwa sasa mpaka watakapomaliza ligi kabisa.
Singida Big Stars imemaliza nafasi ya nne na alama 55, Azam FC ni ya tatu kwa alama 59 huku ikiwa imesalia mechi moja kuhitimisha Ligi Kuu Bara msimu huu.
Pluijm amesema wanahitaji kuimarisha timu kwa ajili pia ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu ujao lakini kwa sasa wanatazamia kumaliza vizuri ligi kisha wageukie mchakato huo aliodai unahitaji umakini mno kulingana na michuano iliyo mbele yao msimu ujao.