Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Pablo awataka Simba kutobweteka

Pablo Simbaz Kocha Pablo

Wed, 16 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BAADA ya ushindi mnono ilioupata klabu ya soka ya Simba kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Pablo Franco amewataka wachezaji wake kutobweteka. Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Asec Mimosas, ushindi ambao umerudisha matumaini ya timu hiyo kusonga mbele hatua zinazofuata.

Akizungumza na HabariLEO kocha huyo raia wa Hispania, alisema bado wana kazi kubwa inawakabili mbele kuhakikisha wanavuka hatua hiyo na kutinga robo fainali, hivyo wachezaji wanajukumu la kuendelea kujituma ili kuhakikisha wanafikia lengo.

“Ni ushindi mnono ukizingatia magumu tuliyokuwa nayo ya majeruhi na kuwakosa baadhi ya wachezaji muhimu, hivyo wachezaji hawapaswi kuendelea kushangilia matokeo hayo sababu bado wana kazi ngumu ya kuhakikisha Simba inasonga mbele, kushangilia tuwaachie mashabiki,” alisema Pablo.

Kocha huyo alisema ushindi huo umekuja katika wakati muhimu na utawasaidia kurudisha ari ya upambanaji na kujiamini pindi wanapokwenda kucheza mechi zao mbili ugenini dhidi ya US Gendarmarie na RS Berkane ya Morocco.

Pablo alisema kitu cha msingi ambacho wanatakiwa kufanya hivi sasa ni kuhakikisha wanacheza kimbinu zaidi ili kuhakikisha hawapotezi mchezo, jambo ambalo litawasaidia kujiweka kwenye mazingira mazuri kwenye kundi lao ambalo kwa sasa linaongozwa na US Berkane na kufuatiwa na Simba.

Alisema ili kufikia malengo atahakikisha kila mchezaji anampangia majukumu yake na kumsimamia kikamilifu kuyatimiza, imani yake ni kwamba kama hilo litatimia, basi uwezekano wa Simba kutinga robo fainali na hata fainali utakuwa mkubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live