Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Pablo ajihami mapema na KMC

Pablo Frano Arrows Pablo Franco Martin

Fri, 24 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa inajiandaa kuwavaa wakusanya ushuru wa Manispaa ya Kinondoni KMC jioni ya leo katika dimba la Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora, Simba SC imechukua tahadhari zote dhidi ya wapinzani wao.

Mchezo huo wa Ligi Kuu NBC, utapigwa majira ya saa 10:00 jioni, lakini Kocha wa Simba Pablo Martin anafahamu fika ubora wa wapinzani wao.

Kocha Pablo anasema;

"Mchezo utakua mgumu sababu KMC wana Kikosi kizuri, na lazima kuwa nao makini. Bado kuna baadhiya wachezaji wetu hawapo vizuri lakini tunaangali nini cha kufanya " amesema Pablo

Simba inahitaji ushindi kwa udi na uvumba ili kupunguza pengo la alama baina yao na vinara wa Ligi Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live