Kocha Mkuu wa PSG Christophe Galtier amewekwa chini ya ulizi wa polisi kwa mahojiano pamoja na mwanawe kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya ubaguzi, mwendesha mashtaka wa Nice aliambia AFP siku ya Ijumaa.
Hatua hiyo inafuatia uchunguzi ulioanzishwa mwezi Aprili, kufuatia madai kwamba alitoa matamshi ya ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu kuhusu wachezaji alipokuwa akiifundisha OGC Nice msimu wa 2021/22.
Galtier anatazamiwa kutimuliwa na wamiliki wa PSG wa Qatar baada ya kutopata matokeo mazuri ambapo PSG ilipokea vipigo 10 msimu wa 2022- 23, na kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 bora na Bayern Munich mabo 3-0 nyumbani na ugenini