Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha PSG amtaja Dembele, asema hili..!

Dembele PSG Kocha PSG amtaja Dembele, asema hili..!

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya PSG Luis Enrique amezungumza na kumsifia winga wa klabu hiyo kua ni mchezaji mzuri na kusema kua kama angekua shabiki wa timu nyingine angelipa tiketi kwajili ya kumuona Dembele.

Kocha Luis Enrique ameyasema hayo baada ya mchezo wa jana wa klabu ya PSG kupata matokeo ya ushindi katika mchezo wao wa kwanza wa ligi ya mabingwa msimu huu.

Kocha huyo amesema Dembele ana ubora wa kitofauti anaweza akakosa nafasi tatu lakini bado anavutia kumuangalia, Jambo ambalo linaonesha kocha huyo ana matumaini makubwa kwa mchezaji huyo.

Winga Ousmane Dembele amecheza michezo saba katika mashindano yote ndani ya klabu ya PSG mpaka sasa, Lakini hajafanikiwa kufunga bao wala kutoa pasi ya bao katika mchezo hata mmoja mpaka sasa.

Licha ya Dembele kutokufunga wala kusaidia upatikanaji wa bao katika michezo saba aliyocheza ndani ya PSG mpaka sasa, Lakini kocha Luis Enrique bado ameendelea kuonesha imani kubwa juu ya winga huyo kwa kumsifu hadharani licha ya kutokuonesha ubora mkubwa ndani ya timu hiyo mpaka sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live