Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Nzoia Sugar alilia nyota wake

Salim Babu Kocha wa klabu ya Nzoia Sugar FC, Salim Babu

Sat, 18 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Nzoia Sugar FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kenya FKFPL Salim Babu amesema anatamani wachezaji wa kikosi hicho wabakie klabuni hapo ili aendelee kufanya vizuri kunako KPL.

Matamanio ya kocha Babu ambaye amewai kuinoa klabu ya Kisumu All Stars yamekuja ikiwa ni baada ya timu hiyo kufanya vizuri na kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Kenya na wachezaji wake wengi kuanza kumendewa na miamba ya soka nchini humo.

Dirisha dogo la usajili linakaribia kufunguliwa na kuna uwezekano wachezaji wengine wakaondoka klabuni hapo ambapo Babu amesema anatamani wasiondoke mpaka mwishoni wa msimu.

“Nimekuwa nikiongea nao kuwaomba wasiondoke mpaka mwishoni wa angalau msimu huu. Nimekuwa nikiwaambia wabakie hapa tufanye vizuri tutapata ofa nzuri zaidi hapo baadaye”, alisema Babu, kocha wa Nzoia Sugar ambao wana pointi 33.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live