Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Nigeria: Bafana Bafana ni Hispania watupu

Bafana Mamelodi Kocha Nigeria: Bafana Bafana ni Hispania watupu

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Nigeria, Jose Peseiro amesema amevutiwa na namna klabu ya Mamelodi Sundowns ilivyoibeba timu ya taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’.

Kikosi cha Kocha Hugo Broos cha Bafana Bafana kina wachezaji 10 kutoka Mamelodi Sundowns na itaivaa Nigeria katika nusu fainali ya michuano hiyo usiku huu.

Akikumbushia namna timu ya taifa ya Hispania ilivyoshinda Kombe la Dunia 2010, ikiwa na kikosi kilichojaa wachezaji wa Barcelona, Peseiro alizifananisha timu hizo mbili na akasifu vijana wa Mamelodi Sundowns walivyoamua staili ya kucheza ya Bafana.

“Timu hii imeonyesha muunganiko mzuri sana. Hawachezi soka Ulaya, lakini wanacheza katika klabu moja,” alisema Peseiro kuiambia tovuti ya FARPost.

“Nakumbuka jinsi Hispania ilivyochezesha wachezaji wa kabu moja, nyota saba kutoka Barcelona na watatu kutoka Real Madrid. Timu ya taifa ya Hispania ilionyesha muunganiko bora kabisa kwa sababu wachezaji walikuwa wakicheza pamoja klabuni Barcelona kwa miaka kadhaa.

“Timu ya taifa ya Afrika Kusini ina wachezaji tisa (kiuhalisia ni 10) kutoka katika timu moja; Mamelodi Sundowns,” kocha huyo Mreno aliongeza.

“Kama timu itachezesha wachezaji hao hao, angalau tisa katika mechi ya kwanza na wachezaji pamoja klabuni kwa mwaka ama miaka miwili, hakika wanaboresha muunganiko.

“Timu hii ya Afrika Kusini imeonyesha muunganiko wa kipekee kabisa, wanakaba maeneo, ni mara chache kuacha mianya.”

Mwendo mzuri wa Bafana kwenye Afcon tayari umeamsha mijadala Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL) ndio ligi bora Afrika kwa sasa.

Katika mechi nyingi za Afcon kocha Hugo Broos alikomaa na mpango wake wa kuwaanzisha wachezaji wanane wa Mamemoldi Sundowns katika kikosi cha kwanza na usiku huu wanaanza sita.

Kikosi hicho kimehusisha wachezaji wote watano wa safu ya ulinzi kutoka kwa chama la ‘Masandawana’, akiwamo kipa Ronwen Williams aliyeokoa penalti nne katika robo fainali dhidi ya Cape Verde.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live