Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Nabi kutakiwa Timu ya Taifa, Mzee mpili awapa onyo TFF

Mpili Nabi Mzee Mpili amegoma Nabi kuondoka Yanga

Wed, 1 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Taarifa kusamba za Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi kuhitajika na Shirikisho la Mpira TFF kuchukua mikoba ya kuinoa Timu ya Taifa Taifa Stars.

Tayari taarifa hizo zimeibua taharuki kwa wapenzi na Wananchama wa klabu ya Yanga juu ya Kocha wao.

Mwananchama wa Klabu ya Yanga, Mzee Mpili amewataka TFF kutafuta Kocha mwingine wa kuinoaTimu ya Taifa "Taifa Stars" na sio Kocha wao Nasreddine Nabi kama tetesi zinavyosambaa kwenye mitandao ya Kijamii.

Akizungumza katika Makao Mkauu ya Klabu ya Yanga leo Machi 1, Mze mpili amesemawashukia Viongozi wa TFF kwa ukali akisema;

" Sisi Tunamtegemea Kocha wetu Nabi. Wao watafute Kocha mwingine, waingie Google watafute Kocha wa Nchi yoyote wampe kazi. Kuhusu Nabi wasahau kabisa suala hilo"

" Pesa wanazo kama sivyo watafute hata Makocha wa ndani wapo kina Boniface (Mkwasa) wasituharibie mfumo, kuhusu Nabi wasahau kabisa wala wasiwe na ndoto nalo"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live