Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Nabi afunguka kufutwa kazi Yanga

NABI KOCHA MKUU YANGA FD Kocha Nabi afunguka kufutwa kazi Yanga

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nassredine Nabi, amefunguka rasmi suala lake la kufukuzwa kazi ndani ya timu hiyo.

Ndani ya Yanga, kumekuwa na taarifa za kufukuzwa kwa makocha wawili wa timu hiyo, Nassredine Nabi na Cedric Kaze, jambo ambalo Championi Jumatano limebidi kumtafuta Kocha Nabi ili kufahamu undani wa taarifa hizo.

Jana Nabi alikuwa kwenye mkutano na Waandishi wa Habari akizungumzia maandalizi ya mchezo wa Yanga dhidi ya KMC utakaopigwa leo Jumatano kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar na waandishi walipojaribu kumuuliza kuhusu kufutwa kazi aliwakatisha na kutaka kuzungumzia mechi hiyo.

Awali Nabi alitishia kugoma kuzungumza na Wanahabari kwa madai ya kutokuwepo kwa mkalimani wake ambaye amekuwa akimtafsiria kutoka Kifaransa kwenda Kiswahili, lakini baadaye alikubali kuzungumza baada ya mwandishi kujitolea kutafsiri kile ambacho alipanga kuzungumza.

Kuhusu mchezo wa leo, Nabi alisema: “Tumejiandaa vyema kwa ajili ya kukabiliana na KMC, malengo yetu kwa sasa ni kuhakikisha tunapata matokeo mazuri, tunajua wapinzani wetu ni bora, hivyo lazima tujitahidi kupambania pointi 3 muhimu.”

Championi Jumatano, lilimganda Nabi kutaka kuujua ukweli wa yeye kufutwa kazi ambapo alipomaliza tu mkutano akadakwa na waandishi wa gazeti hili nje ya Ofisi za Benki ya NBC zilizopo Posta, Dar, sehemu ambayo mkutano huo ulifanyika ili kuujua ukweli kutoka kwake.

Nabi aliyeonekana hana furaha usoni mwake sambamba na kuonekana kuwa na manung’uniko tofauti na siku zingine, aliomba kuzungumza kwa kifupi kuhusu nini kinaendelea kwenye kibarua chake Yanga.

Nabi raia wa Tunisia, alisema: “Sijapewa taarifa rasmi na uongozi wa Yanga kama natakiwa kuondoka, mimi nachofahamu kwa sasa bado ni kocha wa Yanga na ndio maana utaona ni kwa kiasi gani nipo katika mkutano na waandishi kuelekea mchezo wetu na KMC.

“Kama itatokea kuwa nimeondolewa basi ni sawa kwa kuwa ndio mpira ulivyo, lakini kwa sasa hakuna taarifa rasmi ambayo nimepokea kutoka kwa viongozi wangu kuhusiana na mimi kuondolewa Yanga.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live