Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Nabi: Bacca ameleta unafuu Yanga

Bacca X Nabi Bacca na Nabi

Tue, 23 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Achana na rekodi iliyowekwa na Yanga kutinga fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuing'oa Marumo Gallants ya Afrika Kusini, habari ya mjini ni safu ya ulinzi ya mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara, huku beki kitasa Ibrahim Bacca akitajwa kuleta unafuu flani kikosini kwa sasa.

Yanga inayonolewa na Nasriddine Nabi imecheza jumla ya dakika 630 na kuruhusu bao moja tu tangu ilipoanza kumtumia Ibrahim Bacca kwenye beki ya kati mara ilipotoka sare ya 1-1 ugenini hatua ya makundi ya michuano hiyo na Real Bamako ya Mali na kufanikiwa kutinga fainali ikiwa ni rekodi.

Ukuta wa Yanga kwa sasa upo chini ya makipa Djigui Diarra na Metacha Mnata, mabeki Kibwana Shomari, Djuma Shabani, Joyce Lomalisa, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Abdallah ‘Bacca’ wakicheza kwa maelewano makubwa na tangu ilipotoka sare ya 1-1 ugenini ilicheza mechi hizo saba mfululizo za CAF ikifungwa bao moja katika matokeo ya Jumatano iliyopita dhidi ya Marumo iliyowafumua kwao 2-1 na kufuzu kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-1.

Mechi hizo hizo saba ni dhidi ya Real Bamako (2-0), US Monastir (2-0), TP Mazembe (1-0) zikiwa makundi kisha kutinga robo fainali na kupta matokeo dhidi ya Rivers United 2-0 na 0-0 kabla ya kutinga nusu fainali na kuvaana na Marumo iliyowachapa 2-0 nyumbani kisha kushinda ugenini 2-1.

Kabla ya mechi hizo Yanga ilicheza tano zikiwamo mbili za play-off na tatu za makundi iliruhusu mabao manne, ikiwamo kufungwa 2-0 ugenini na US Monastir kisha kushinda 3-1 dhidi ya TP Mazembe na sare ya 1-1 Real Bamako, huku mabao iliyofungwa ikiwa ni ile ya mipira iliyokufa.

Hata hivyo, akizungumza nasi kabla ya kwenda Singida katika mechi ya nudu fainali ya ASFC, Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi alisema ana mabeki bora ambao wanacheza kwa umoja na maelewano makubwa ndio siri kubwa ya wao kuweza kuwa na rekodi nzuri kwenye mashindano hayo ambayo ameweka wazi kuwa bado wanasafari ndefu ili kuweza kufikia malengo.

"Kuna mabadiriko makubwa safu yetu ya ulinzi, kwa sasa ipo makini na imepunguza makosa madogo madogo yaliyokuwepo na uwepo wa Bacca pia umekuwa imara kutokana na kuwa makini na mipira ya juu changamoto iliyokuwa ikituumiza sasa inaonekana kuondoka," alisema Nabi na kuongeza;

"Mabeki wetu wanacheza kwa umoja, wanaendeleza kile tunachowaelekeza mazoezini ni furaha kuwa nao kwa pamoja na naamini wanazidi kuimarika na kuelewana siku hadi siku.”

Nabi alisema walikuwa wakifungwa sana mabao ya mipira ya kutengwa lakini sasa tatizo hilo analiona linapungua anaamini uwepo wa Bacca na kusogezwa kwa Yanick Bangala namba sita kumeongeza umakini kwenye safu yake ya ulinzi.

Baada ya kummtafuta Bacca ambaye amepata bahati ya kucheza michuano ya kimataifa na kuonyesha ubora ukiwa ni msimu wake wa kwanza, naye alisema juhudi zake na uelewano mzuri na wachezaji wenzake ndio siri ya ubora wake.

"Ubora wa Yanga ndio umenifanya niwe imara umenipa changamoto ya kujiandaa vizuri kiakili na uwezo wangu binafsi ili Beki ni eneo linalohitaji umakini wa hali ya juu kwani ukikosea tu unaweza kuigharimu timu. Nilivyokuja Yanga niliwakuta mabeki hawa wakicheza vizuri na kujipa muda wa kupata nafasi na sasa nashukuru ninacheza,” alisema Bacca na kuongeza;

“Nadhani siri kubwa ni kujituma na kujitoa kwaajili ya timu, ukituangalia wote tunafanya hivyo na kila mmoja kwa nafasi yake anahakikisha hafanyi makosa na hata yakitokea basi anayasawazisha kwa haraka au mwingine anafanya hivyo. Nadhani umoja wetu ndio siri kubwa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: