Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Mtibwa Sugar aifungia kazi Young Africans

Zuberi Katwila Mtibwa.png Kocha Mtibwa Sugar aifungia kazi Young Africans

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema anakerwa na muendelezo wa matokeo mabovu inayopata timu hiyo Ligi Kuu na sasa anautolea macho mchezo dhidi ya Young Africans.

Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa Young Africans Jumamosi (Desemba 16), katika Uwanja wa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam.

Katwila ndiye kocha pekee kuondoka na pointi tatu dhidi ya mabingwa wa soka Tanzania Bara msimu huu pale alipoiongoza Ihefu kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 Uwanja wa Highland Estate, Mbarali, Mbeya.

Mtibwa imepoteza mechi tano mfululizo kwenye Ligi Kuu dhidi ya KMC bao 1-0, JKT Tanzania 2-1, Azam FC 5-0, Tabora United 2-1 na Namungo 1-0 na kuwa mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi tano.

Kocha Katwila amesema kuwa kama kocha hafurahishwi kabisa na kipindi anachopitia hivi sasa baada ya kushindwa kupata pointi kwenye michezo mitano iliyopita, hivyo anarudi kujipanga kwa ajili ya michezo ijayo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Amesema kuwa huu ni wakati wa timu yake kushikamana pamoja na kuangalia madhaifu yao kitaalamu zaidi kabla ya kushuka uwanjani tena kuzisaka pointi tatu zitakazorudisha morali yao.

Chanzo: Dar24