Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Morocco yamkuta ya Adel Amrouche AFCON

Walid Regragui Kocha Wa Timu Ya Taifa Ya Morocco Kocha wa Morocco, Walid Regragui

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Tanzania ikiendelea kumkosa kocha wake Adel Amrouche aliyefungiwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Morocco nao wakumbana na rungu hilo baada ya kocha wao Walid Regragui kufungiwa.

Kikao cha kamati hiyo kilichoketi leo kimemkuta na hatia Regragui baada ya kukwaruzana na nahodha wa DR Congo Chancel Mbemba.

Regragui amefungiwa mechi nne sambamba na faini ya Dola 5,000 kufuatia vurugu hizo ambazo zilizuka zaidi mara baada ya mpira kumalizika baina ya timu hizo.

Hata hivyo Shirikisho la Morocco limetoa taarifa kwamba litakatia rufaa adhabu hiyo ya Regragui ambaye anakuwa kocha wa pili kufungiwa akitanguliwa na Amrouche wote wakiwa kwenye kundi Moja F kwenye Fainali hizo zinazoendelea nchini Ivory Coast.

Chanzo: Mwanaspoti