Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Morocco aupa tano Uwanja wa Mkapa

Kocha Morocco X Uwanja Kocha Morocco aupa tano Uwanja wa Mkapa

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Morocco, Walid Regragui amesema kwamba kitu pekee amekipenda tangu amekuja Tanzania kwaajili ya mchezo wao dhidi ya Taifa Stars ni uwanja mzuri wa Benjamin Mkapa ambapo ndipo kesho saa 4 usiku itakapopigwa mechi yao ya Kufuzu Kombe la Dunia 2026

"Katika maisha yangu ya Ukocha naweza sema kitu kinachonikwaza awali kabla ya mchezo ni Uwanja, nikishauona tu haufai huwa sina amani tena.. viwanja baadhi ya Afrika sio vizuri lakini kwa Tanzania naona hiki cha kwao wamejitahidi.."

"Nilikuja nikiwa siifahamu Tanzania kwasababu ndio mara ya kwanza nafika hapa ila naweza sema kwa muda mchache niliokaa tayari nimeona hii palivyo.. pana hali ya hewa nzuri na sijui ni hiki kipindi tulichokuja sisi au ndio panakuwaga hivi mwaka mzima."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live