Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Morocco: Wamorocco hawapaswi kuumia bali kufurahia

Walid Acram Wamorocco hawapaswi kuumia bali kufurahia

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndoto ya pengine kushinda Kombe la Dunia kwa mwaka 2022 kwa Morocco imemalizika siyo kwa huzuni bali imetimizwa.

Ilikuwa vigumu Novemba 21 kwa mtu yeyote kutabiri hiki ambacho kimetokea kwa Morocco, si ajabu wachambuzi na wadau wa soka nchini na hata kwenye maeneo mengi wangetaja timu kama Senegal ambayo imesheheni majina mazito katika uga wa mpira wa miguu Ulaya.

Morocco imeibuka kutokea kusikojulikana na kufanya kila mmoja kugeuza macho na kuitazama kwa namna ya kipekee hasa baada ya mchezo wa hatua ya 16 bora, robo fainali na hata nusu fainali.

Kocha Walid Hoalid Regragui alisimama kidete katika hilo. Alikuwa na mbinu ambazo mara zote zimemlipa vilivyo. Mechi mbili za mtoano (Hispania, Ureno) aliingia kwa kujilinda, alishambulia kwa kujibu. Mechi ya nusu fainali na Ufaransa waliingia kwa kushambulia. Mwanasoka ambaye alitazama mchezo huo atakwambia Ufaransa wameshinda lakini cha moto wamekiona.

Pamoja na kupoteza kwa bao 2-0 dhidi ya Ufaransa kwa magoli ya Theo Hernandez na Muani, kocha Regragui anasema siyo wakati wa kuumia bali kufurahia.

“Tulifanya kila liwezekanalo kuhakikisha tunashinda mchezo lakini haikuwa hivyo. Hatupaswi kujutia bali kufurahia tulichokipata. Ni mafanikio makubwa kwetu”, alisema Regragui kocha wa zamani wa klabu ya Wydad Casablanca.

“Hauwezi kushinda Kombe la Dunia kimaajabu, kwa bahati mbaya, utashinda tu kwa kujituma na hicho ndicho tulichokuwa tunakifanya”.

Mashabiki wa Morocco ni sehemu nyingine ya ndoto hiyo kufika hapo kwani “vibe” lao lilikuwa la kipekee. Mechi ya nusu fainali ilikuwa mara mbili kwani hata idadi iliongezeka.

Mashabiki walishabiki na kuwapa nguvu wachezaji kiasi kwamba hata Morocco walipokuwa nyuma kimatokeo haikuwa rahisi kugundua hilo.

Kwa sasa tumaini lililobakia kwa Simba wa Milima ya Atlas ni kuwa mshindi wa tatu kwa kuifunga Croatia katika mchezo wa kuwania nafasi hiyo utakaochezwa Disemba 17 siku ya Jumamosi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live