Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Mmisri anukia Kitayosce

Kitaysce Pic Kocha Mmisri anukia Kitayosce

Wed, 14 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya Kitayosce kuachana na Kocha wake Mkuu, Kefa Kisala aliyejiunga na Fountain Gate mabosi wa timu hiyo nao wanataka kumchukua Mmisri, Ahmed Soliman akakiongoze kikosi chao.

Mabosi wa Kitayosce wanataka kuitumia nafasi hiyo kumrudisha tena Soliman ambaye taarifa zinadai alikuwa anamalizana na Fountain kwa ajili ya masilahi yake ili aweze kurudi kwao.

Akizungumza Mkurugenzi wa klabu hiyo, Yusuph Kitumbo alisema wapo makocha wengi walioomba nafasi hiyo lakini bado hawajafikia maamuzi ya mwisho wampatie nani timu yao.

“Wapo wengi ambao wameonyesha kuihitaji timu yetu na kwa kweli inaonyesha ni kwa jinsi gani tunafuatiliwa, suala la nani atapewa hilo tusubiri tu maamuzi ya mwisho,” alisema.

Licha ya kauli ya Kitumbo ila Mwanaspoti linatambua Soliman ndiye amepewa mikoba hiyo na jana ndiye aliyesimamia mchezo wa Kombe la Azam (ASFC) hatua ya pili dhidi ya Namungo FC.

Soliman alitua Tanzania Februari 12 mwaka huu na alimaliza msimu akiiacha Fountain Gate nafasi ya nane na pointi 42 baada ya kucheza michezo 30 ikishinda 11, sare tisa na kupoteza 10.

Kwa msimu huu wa 2022/23 ameiongoza kwenye michezo 12 akishinda minane na kupoteza minne akikiacha kikosi hicho kikiwa nafasi ya nne baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 24.

Chanzo: Mwanaspoti