Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Middendorp aisoma Future FC

Image 113.png Kocha Middendorp aisoma Future FC

Sun, 10 Sep 2023 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu mpya wa Singida Fountain Gate FC, Middendorp, kufanyia kazi ubora wa wapinzani wao katika mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika, Future FC kutoka Misri.

Singida Fountain Gate ambayo ipo Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa hatua ya kwanza utakaochezwa Septemba 17, mwaka Ernest ameanza huu kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Hussein Masanza, amesema Kocha Middendorp ameshaanza kazi na anaonekana zaidi anawajenga viungo ili kuwaweka tayari kuwakabili Waarabu hao kutokana na uwezo waliokuwa nao.

Masanza amesema kocha huyo anaamini muda uliopo utamsaidia kukiimarisha kikosi chake huku tayari ameshafahamu baadhi ya nyota tegemeo wanaotakiwa kuchungwa katika kikosi cha Future akiwamo, Ahmed Refaat, ambaye anaweza kucheza winga zote mbili na kiungo mshambuliaji.

Amesema baada ya benchi la kufatilia video za michezo mbalimbali ya kimataifa walizocheza hivi karibuni, wamebaini wachezaji sita waliokuwa hatari wameondoka katika timu hiyo.

“Kocha amefanikiwa kuwafuatilia Future na kuona ubora wao, amewajua baadhi ya wachezaji ambao ni roho ya timu, wako imara kwenye safu ya kiungo (Refaat) ambaye anekuwa akisumbua sana kwenye mechi zilizopita,” amesema Masanza.

Ameongeza wanaendelea kufanyia kazi mapungufu ya timu yao yaliyojitokeza katika mechi zilizopita ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele.

“Future FC ni wazuri, tunajiandaa vyema kuwakabili kwa sababu tutaingia uwanjani kama underdog, tunawaheshimu wapinzani wetu kulingana na ubora waliokuwa nao,” Masanza amesema.

Kuelekea mchezo huo wa kimataifa, kikosi chake kinatarajia kujiimarisha kwa kucheza mechi mbili ngumu za kirafiki na huenda leo Jumamosi (Septemba 09) ikavaana na Maafande wa JKT Tanzania.

Chanzo: Dar24