Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Mfaransa: Namtaka Aziz Ki wa Yanga

Aziz KI 9 Goals Aziz Ki.

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna mastaa watatu wanaocheza Ligi Kuu Bara wamesalia kwenye fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) zinazoendelea huko Ivory Coast, akiwamo kiungo mshambuliaji Stephanie Aziz KI wa Burkina Faso, ambapo kocha wa timu hiyo amekiri anamvuruga, huku akitamka kitu kuhusu Yanga anayoichezea.   Aziz KI anaongoza kwa ufungaji Ligi Kuu akiwa na mabao 10 kupitia mechi 11 kabla ligi haijasimama kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024 na Afcon.

Kocha wa Burkina Faso, Hubert Velud wanaojiandaa kuvaana na Mali katika hatua ya 16 bora inayoanza leo, aliliambia Mwanaspoti kuwa Aziz KI ni mmoja wa viungo mafundi wa boli, lakini katika kikosi hicho bado hajampata kama yule anayemuona akiwa Yanga.

Velud, raia wa Ufaransa alisema anatamani kumuona Aziz KI mwenye makali kama anavyokuwa akiwa Yanga, lakini kiwango hicho kimeshindwa kuonekana akiwa na jezi ya Burkina Faso.   “Kuna kitu natamani kukiona zaidi kwa Aziz KI akiwa na timu ya taifa. Tangu nimefika hapa nimekuwa nikimuita, lakini kile ambacho anakionyesha akiwa na klabu yake bado sijakiona sawasawa hapa,” alisema Velud.   “Huyu ni mmoja kati ya viungo washambuliaji bora sana. Ana kipaji kikubwa, lakini naona kama akiwa klabuni kuna makali anayaacha kule akiwa anakuja huku. Tunaendelea kufanyia kazi ubora wake ulete matunda zaidi akiwa huku timu ya taifa. Nahitaji kitu kikubwa zaidi (kutoka kwake) siku tukikipata tutacheza mpira wa kiwango cha juu sana.”

Velud alikiri kuwa licha ya Aziz KI kuzitendea haki dakika ambazo amepewa kwenye mechi tatu za makundi, lakini akadai kushindwa kuelewana na washambuliaji wa timu hiyo ya taifa ni changamoto.   “Kwa muda ambao amecheza kuna kitu amefanya, lakini mimi sio aina ya makocha ninayeridhika na matokeo madogo. Kuna wakati tunaona kwamba shida ipo, bado kuna muunganiko hajaupata na watu wa mbele hasa washambuliaji. Kuna pasi zake zimeshindwa kutumika sawasawa,” alisema.   “Wakati mwingine hizi ndizo changamoto tunazokutana nazo. Wachezaji wanapokuja kukutana kwa muda mfupi timu za taifa, tofauti na wanapokuwa kwenye klabu zao.”

Aziz KI anakwenda kupunguzana na kipa wa Yanga, Djigui Diara kuwania tiketi ya kucheza robo fainali kwenye mechi  ya Januari 30 Mali itakapokutana na Burkina Faso.

Staa mwingine aliyesalia kwenye fainali hizo ni beki wa Simba na DR Congo, Hennock Inonga ambaye atachuana dhidi ya Misri Januari 28.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live