Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Mexime atua Ihefu FC, atoa kauli nzito

Mecky Maxime Best Coach Kocha Mexime

Thu, 28 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mpya wa Ihefu, Mecky Mexime amesema ndio kwanza amekabidhiwa kazi, atakapoanza majukumu rasmi, atajua aanzie wapi kwa maana ya mbinu ama kuongeza watu dirisha dogo.

Mexime amefanya mahojiano na Mwanaspoti ambapo amefunguka namna kazi yao ilivyo ngumu, lakini hawana budi kupambana kuhakikisha Ligi Kuu Bara inakuwa bora.

"Ili mbinu za kocha zijulikane ni bora, lazima asaidie timu kwenye mazingira magumu, hivyo nakwenda kupambana, naamini mambo yakakwenda vizuri," amesema

Mexime amejiunga na timu hiyo, akitokea Kagera Sugar, ikiiacha nafasi ya 14 katika mechi 13 imeshinda tatu, sare nne na imefungwa michezo sita, imefunga mabao manane, imetikiswa nyavuni mara 16 na ina pointi 13.

Mexime ana kazi kubwa ya kufanya ndani ya timu yake mpya ambayo ipo nafasi ya 13 katika mechi 14, imeshinda tatu, sare nne, imefungwa saba, ina pointi 13, inamiliki mabao 10 na imefungwa mabao 17.

Si jambo linalomtisha kocha huyo, kwani amesisitiza kazi yake ni kufundisha anaamini kila kitu kitakwenda sawa.

Ndani ya Ihefu msimu huu, Mexime atakuwa kocha wa tatu, alikuwepo Zuberi Katwila ambaye kwa sasa yupo Mtibwa Sugar na Moses Basena kutoka Uganda ambao waliondolewa.

"Ligi ni ngumu, lakini hakuna kitu rahisi zaidi ya kupambana, naamini kila kitu kitakuwa sawa," amesema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live