Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Mexico aachia ngazi

Gerardo 'Tata' Martino Gerardo 'Tata' Martino

Thu, 1 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuboronga kwenye fainali za Kombe la Dunia yanayoendelea huko Qatar, kocha aliyekuwa akiinoa Mexico, Gerardo 'Tata' Martino ameachia ngazi Shirikisho la soka Mexico limetoa taarifa.

Kwenye fainali hizi za Kombe la Dunia Qatar, Mexico ilianza kwa sare dhidi ya Poland kabla ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Argentina baadaye ikaambulia ushindi dhidi ya Saudi Arabia hatua ya makundi hata hivyo ikashindwa kutoboa raundi ya 16 bora.

Mara ya mwisho Mexico kushindwa kutinga raundi ya 16 bora ilikuwa kwenye fainali za Kombe la Dunia yaliyofanyika mwaka 1978.

Akizungumza baada ya kuachana na timu hiyo licha ya Mexico kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, kocha huyo alisema "Ninahusika na matokeo haya mabovu, mkataba wangu umemalizika baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa, hakuna kitu kingine cha kufanya baada ya hapa,"

Ushindi wa mabao 2-1 kwa upande wa kocha wa Mexico haukuwa na maana kwake kwani timu yake ilikuwa kataika hali mbaya baada ya kuboronga mechi zao za mwanzo dhidi ya poland na Argentina.

Tata aliteuliwa kuwa kocha wa Mexico tangu mwaka 2019 na Shirikisho la Soka Mexico, kabla yakuinoa timu hiyo alikuwa na uzoefu wa kuzinoa timu nyingine za taifa za Uruguay na Argentina.

Aliwahi kuzipeleka Argentina na Uruguay kwenye fainali za Kombe la Copa America mwaka 2011, 2015 na 2016. Katika ngazi ya klabu Tite aliwahi kuzinoa Newell's Old Boys, Barcelona na Atalanta United.

Chanzo: Mwanaspoti