Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Medeama: Yanga wametunyima Uwanja wa kufanya mazoezi

Kocha Mkuu Wa Medeama,Evans Augustin..jpeg Kocha mkuu wa klabu ya Medeama ya nchini Ghana Evans Augustin

Tue, 19 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa klabu ya Medeama ya nchini Ghana Evans Augustin amelalamika kuwa wamenyimwa uwanja wa kufanyia mazoezi tangu wamefika hawajafanya mazoezi.

"Tangu tumekuja tumeshindwa kufanya mazoezi, tunajikuta tunafanyia mazoezi hotelini.

"Tumekosa uwanja wa kufanyia mazoezi sijajua ni kwanini, ila hii ni changamoto ambayo tumekutana nayo ila sijui kwanini tumekosa, zipo ishara zinazoonyesha kuwa tumenyimwa". Amesema Kocha Mkuu wa Medeama SC, Evans Augustin.

Medeama itacheza na Yanga kesho kwenye mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika hatua ya makundi katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar Es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: